Wednesday, 26 August 2015

Kinachoendelea Hyatt Regency Hotel: Majadiliano kuhusu Amani na Usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu, 2015.

Leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar, wawakilishi wa Vyama vya Siasa, Msajili wa Vyama vya Siasa na wadau wa Amani na Usalama, wanajadiliana kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015

-Pia wanajadili vikundi vya Ulinzi na Usalama vya vyama vya Siasa kuelekea uchaguzi Mkuu


Leo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na moja ya wafadhili wa mtandao huo Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA). unaendesha mkutano katika Hoteli ya Kilimanjaro ya Jijini Dar es Salaam mafunzo yatakayowakutanisha Tume ya Haki za Bindamu na Utawala Bora nchini, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, Jaji Mkuu wa Mahakaam Kuu ya Tanzania na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi,

Washiriki wengine ni pamoja na Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa (THRDC), Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, Katibu Mkuu wa CCM, Nape Nauye, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) BAKWATA, Dr. Benson Banna (TEMCO), Peter Kuga Mziray- Mwenyekiti wa Chama cha APPT Maendeleo, Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) ,Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Chama Cha ACT Wazalendo na Chama Cha NCCR-Mageuzi wamethibitisha kushiriki mafunzo hayo.

Aidha, pamoja na mambo mengine wanajadili mada juu ya dhana ya usalama katika kupindi cha uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuangalia suala la usalama kuwa lilizingatiwa kiasi gani, pamoja na kuangalia changamoto za uchaguzi huo ili kwa pamoja waweze kujadiliana kwa pamoja changamoto zinazoweza kujitokeza/kuepukwa zinazoweza kuchochea ghasia kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba, 25, 2015.


-J. Jesse, kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaamm, amesema vikundi vya Usalama vya vyama vinafanya hadi kazi ya kukamata, kuhoji na kuadhibu watu. Ni tishio la Usalama wakati huu

Amesema baadhi ya vyama vilivyohojiwa vilidai havina imani na Jeshi la Polisi, uwepo wa vikundi hivi ni kinyume na Katiba.

-Kwa sasa anazungumza Salum Mwalimu (CHADEMA), anasema suala la Vikundi vya Vyama na Suala la Ulinzi & Usalama ni nyeti. Tunataka uchaguzi ufanyike kwa amani tushike Dola. Suala la Vikundi vya Usalama ktk Vyama bado linazungumziwa kisiasa. Utafiti uko wapi.

Anasema vikundi vya Usalama vya Vyama ni muhimu kwa Usalama wa Viongozi wetu. Mipaka ya Ulinzi wa Viongozi ipoje?.

Amesema wanaodai vikundi vya usalama vya Vyama vinapata mafunzo Kijeshi waseme mafunzo yanafanyika wapi?yeyote anayevunja Sheria akamatwe na ashughulikiwe. Vikundi hivi vipo kwa mujibu wa Katiba za Vyama.

-Mwakilishi CUF: Vikundi vya Ulinzi vya Vyama vilikuwepo tangu zamani; tulikuwa wapi? Hakuna sehemu Katiba inazuia, Katiba za Vyama vyetu zilipishwa na Tume ya Uchaguzi na zinaainisha Uwepo wa Vikundi vya Usalama ktk Vyama.

-Mwanaisha(ADC): Kama Vyama vya Siasa haviruhusiwi kuruhusiwi kuwa na Vikundi vya Usalama, kwanini Katiba za Vyama zilipitishwa?Kama Vikundi vya Vyama vinaruhusiwa, basi viwe na utambulisho kama ambavyo Polisi wanatambulika.
 

No comments: