![]() |
| Celine Dion na Mumewe Rene Angelil |
Kutokana na hilo, mzee Rene amemuomba Mkewe asiwe mbali naye kwani angependa afe akiwa mikononi mwake.
Mwanamuziki mwenye heshima kubwa duniani, Mwanamama Celine Dion (47) amesoneneshwa na kauli ya Mume wake, Mzee Rene Angelil (73) ambayo imewashtua wanafamilia na wadau wa mwanamuziki huyo.
Mzee Rene ameomba afe akiwa mikononi mwa Celine,baada ya kukata tamaa ya kutopona ugonjwa wake wa kansa ambao unamsumbua tangu mwaka jana. Familia ya Celine imehangaika kwa muda mwingi kutafuta tiba lakini madaktari wamesema Mzee Rene hataweza kupona kwani amechelewa kupata tiba
“Nimemuuliza daktari siku gani mume wangu atafariki, lakini daktari amesema hajui, inabidi nijiandae kwa lolote litakalotokea”, alisema Celina.
Celina analazimika kuwa karibu na mume wake ili siku yake itakapofika afie mikononi mwake.Hata hivyo familia hiyo imeweka wazi kwamba wameshakubaliana na hali hiyo hivyo hawanabidi kuendelea na maisha ya amani kwani litakalotokea limepangwa na Mungu.
Celina na Rene walifunga ndoa mwaka 1994 na wamebahatiaka kupata watoto watatu, ambao Nelson Angelil, Eddy Angelil, na Rene-Charles Angelil.

No comments:
Post a Comment