Aliyekuwa mgombea wa kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi jimbo
la mtama SELEMANI METHEW amekihama chama hicho na kuondoka na wana CCM
wapatao miasaba na 4 na kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA kwa kile anachodai hakutendewa haki katika mchakato mzima wa
kura za maoni.
METHEW amesema kuondoka ndani ya CCM kumetokana na maamuzi ya
wananchi ambao wameona haiwezekani na haitawezekana kiongozi
wanayemuitaji kufanyiwa hila na mizengwe,kudhulumiwa haki yake ya msingi
ya kuwaongoza wananchi wa jimbo la mtama.
Amesema jimbo la mtama halihitaji usanii bali linaitaji mgombea
shupavu atakayeweza kupambana na mgombea wa CCM Nape Nnauye huku
akisisitiza uwezo huo anao.
Mkutano huo umeudhuriwa na wanawake wengi ambao kwa sehemu kubwa
ndiyo waliyorudisha kadi za CCM kama anavyofafanua katibu wa chadema
mkoa wa lindi, huku baadhi ya wanaccm wanaeleza sababu za kuondoka na
mgombea huyo.
Mkutano huo ulipambwa na vimbwanga mbalimbali likiwemo tambiko
rasmi lililotumika kumzindika mgombea huyo ikiwa ni pamoja na kumpa
nguvu na kumkinga na majanga ili aweze kufanikisha kampeni na kuibuka na
ushindi.




No comments:
Post a Comment