SIRI kuu ya kujiuzulu uenyekiti katika Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, imeanza kufichuka.
Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
Taarifa kutoka serikalini, ofisi kuu ya CCM, Lumumba, Idara ya Usalama wa taifa (TISS) na kwa watu waliokaribu na Prof. Lipumba mwenyewe zinasema, kiongozi huyo amejiuzulu ili kulinda ajira ya mmoja wa maswahiba wake wakubwa serikalini.
“Prof. Lipumba amejiuzulu baada ya wakubwa ‘kufika bei’ ili kulinda kibarua cha mmoja wa vigogo kutoka idara nyeti serikalini, ambaye ni swahiba wake wa karibu,” ameeleza mmoja wa viongozi wajuu kutoka serikalini.
Haijafahamika kiasi gani cha fedha alicholipwa, ili kumshawishi kujiondoa katika wazifa wake, ingawa kuna taarifa kuwa zaidi ya Sh. 3.7 bilioni zimetumika kwa kazi hiyo.
Aidha, taarifa zinasema, Prof. Lipumba amelazimika kujiuzulu baada ya kuahidiwa madaraka makubwa katika serikali ijayo, ikiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitafanikiwa kushika madaraka ya dola.
Miongoni mwa vyeo ambavyo Prof. Lipumba ameambiwa atakabidhiwa, ni kufanywa kuwa waziri wa fedha katika serikali ya John Magufuli au kuwa mshauri mkuu wa uchumi wa serikali hiyo.
Kupatikana kwa taarifa kuwa Prof. Lipumba amelambishwa donge kubwa ili kusaliti mageuzi, zimekuja siku tatu baada ya mwanasiasa huyo aliyekuwa akiheshimika nchini kutangaza kujiuzulu kwa kile alichoita, “kusutwa na dhamira yake.”
Alisema,
ameamua kujiuzulu wazifa wake wa unyekiti baada ya viongozi wenzake
wanne kutoka jumuiko la vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya
Wananchi (UKAWA), kumkaribisha ndani ya umoja huo, mwanasiasa mashuhuri
nchini, Edward Lowassa na kisha kumteua kuwa mgombea wake wa urais.
Vyama vinavyounda UKAWA, ni NCCR- Mageuzi, CUF, National Democrat League (NLD) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lowassa
alijiunga na Chadema baada ya viongozi wakuu wa UKAWA, akiwamo Pro.
Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Dk. Emanuel Makaidi, kukutana na
kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu jambo hilo.
Vyanzo
vya taarifa vinasema, Prof. Lipumba alikutana mara kadhaa na kwa
faragha na Lowassa kwa lengo la kumshawishi kujiunga na umoja huo.
Miongoni
mwa mikutano hiyo, ni pamoja ule uliofanyika Jumamosi ya tarehe 4
Aprili, majira ya saa 5 asubuhi, ofisini kwa Lowassa, Mikocheni jijini
Dar es Salaam.
Katika
mkutano huo, Prof. Lipumba alimhakikishia Lowassa kuwa UKAWA wako
tayari kumpokea na kumkabidhi bendera yake katika kinyang’anyiro cha
urais cha Oktoba. Alitumia mkutano huo kumkandia Dk. Willibrod Slaa kwa
kudai kuwa siyo mtu mwenye sifa za kuwania nafasi hiyo, kwa madai kuwa
ni mtu asiyeaminika.
Hata
hivyo, Lowassa alimuonya mwanasiasa huyo kuwa makini na kauli zake kwa
kuwa zitaweza kuwagawa. Alisema, anamfahamu vema Dk. Slaa na hana
matatizo naye.
Habari zinasema, mara baada ya Prof. Lipumba kujiuzulu, aliondoka nchini kuelekea Rwanda kwa kazi maalum aliyopewa na CCM.
![]() |
| Picha-hii-imepigwa-jana-toka-Kigali-Rwanda-Prof-Lipumba-na-Wakala-wa-Usalama-kijana-wa-Kinyarwanda. |
Akiongea
na Azam Televisheni, Prof. Lipumba amekiri kuwa nchini Rwnada na
kuongeza, “niko huku kufanya utafiti wa jinsi Rwanda ilivyofanikiwa
kiuchumi,” jambo ambalo linathibitisha madai kuwa atakuwa mshauri wa
uchumi au waziri wa fedha katika serikali ya CCM.
Mtoa
taarifa anasema, Pro. Lipumba ameondoka nchini na walinzi maalum ambao
amekabidhiwa kama sehemu ya makubaliano ya mradi wake na serikali.
Anasema,
“…hii habari ya Lipumba imethibitisha kile nilichokisema siku za nyuma,
Lipumba anatumika. Ni kibaraka… Tena hukutana naye nyumbani kwake.
“Nilipoona
Prof. Lipumba yuko UKAWA nilipata mashaka makubwa, lakini nilikuwa na
ahueni kwa sababu niliambiwa Maalim Seif Sharif Hamad,
alishawatahadharisha wenzake wasimshirikishe Lipumba kwenye mambo nyeti
ya UKAWA kwa sababu haaminiki.”
CHANZO MWANAHALISI ONLINE
CHANZO MWANAHALISI ONLINE


No comments:
Post a Comment