Monday, 10 August 2015

Ukweli kuhusiana na Tetesi za Makamu wa Rais Gharib Bilal kutangaza kukihama chama cha Mapinduzi{CCM}

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Ofisi ya Makamu wa Rais imekanusha taarifa kuwa Makamu wa Rais ataongea na waandishi wa Habari leo kutoa msimamo wake ndani ya CCM.

-Awali jana taarifa zilienea kuwa Makamu wa Rais atakuwa na Mkutano na waandishi wa Habari
 


Ofisi ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

No comments: