Friday, 14 August 2015

Yanga na Azam FC wawazuia wachezaji wao kujiunga na Timu ya Taifa{Taifa Stars}

Kocha wa Timu ya Taifa"Taifa Stars" Charles Boniface
Mkwasa alitangaza kikosi cha timu ya taifa Ijumaa ya August 7 hivyo wachezaji wote wanaocheza Ligi ya ndani ya nchi walitakiwa kuripoti siku ya Jumapili ya August 9.
Wachezaji walioongezwa kikosini ni golikipa Saidi Mohamed, Vicent Andrew, kutoka Mtibwa Sugar, Mohamed Hussein (Tshabalala) na Ibrahim Ajib, kutoka Simba, Hamis Ally na Juma Mbwana kutoka KMKM, Tumba Swed kutoka Coast Union, Samwel Kamuntu kutoka JKT Ruvu na Ibrahim Hilka kutoka klabu ya Zima moto ya Visiwani Zanzibar sambamba na golikipa wa Tanzania Prisons Mohamed Yusuph ambae bado hajawasili kikosini.

 
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Borniface Mkwasa ameamua kufanya maamuzi ya ziada baada ya klabu za Azam FC na Yanga kutowaruhusu wachezaji wake kujiunga na kambi ya Taifa Stars August 9 na badala yake kuendelea na maandalizi yao ya mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa August 22.
DSC_0030
Mkwasa amelazimika kuita wachezaji wapya kumi ili kuendelea na program yake ya mazoezi kama kawaida hivyo hao ambao hawajaruhusiwa kujiunga atawaangalia katika mechi ya Ngao ya Hisani kwani hawezi kumchukua mchezaji ambae hayuko vizuri na labda ana majeruhi ndio maana aliitisha kambi ya siku kadhaa kablaa ya wachezaji kurejea katika vilabu vyao
DSC_0022“Nafikiri ndio hivyo kwa sababu tulitarajia kwamba wiki hii pengine itakuwa sio wiki muhimu sana kwao kwa sababu wana wiki moja mbele ya maandalizi kwa wiki ijayo lakini hatuwezi kuwalazimisha kwa sababu Tanzania ina wachezaji wengi na sisi tuna bank ya wachezaji kama wamewazuia basi tutawachukua wengine kama unavyoona”>>>Mkwasa
DSC_0030


Zaidi Mkwasa ameongea hapa

No comments: