Monday, 14 September 2015

MSANII NAY WAMITEGO AIBIWA WALLET LILILOKUWA NA KIKATIO CHAKE{KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA}

Nay Wamitego
Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard Nay Wamitego alisema kuwa siku hiyo alikuwa maeneo ya Mwenge kupeleka gari la mama yake ‘garage’ kwa ajili ya kulifanyia ‘service’.
‘’Siku hiyo nilikuwa nimetoka safari kabla sijaondoka nilikuwa nimemnunulia mama yangu gari kwa ajili ya kutembelea ni gari ndogo lakini niliwaacha wadogo wangu wakaenda kuichukua,siku ambayo nikuwa nimerudi walikuja kunifuata na hiyo hiyo gari ndogo,’’alisema Nay.
‘’Kwahiyo walivyokuja kunifuata nikaona wacha tuipeleke ‘garage’ kuifanyia ‘service’ kwahiyo tukatoka pale hadi maeneo ya Mwenge kwenye ‘garage’ Fulani hivi huwa wanafanya service,mafundi walikuwa wanafunga ‘tinted’ kabla ya kumwaga ‘oil’ akapita dada mmoja muuza juisi nikamuita nikanunua juisi,wakati nakunywa hiyo juisi pia nilikuwa naongea na simu,’’aliongeza Nay.
‘’Nilikuwa naongea na mwanangu mkubwa wa kwanza aliyekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu nilikuwa sijaongea naye,wakati naongea nilikuwa nimeweka miguu juu ya ‘dashboad’ na niliona wakati ‘wallet’ yangu ikianguka kwenye gari lakini nikasema nikimaliza kuongea nitaiokota mwisho wa siku Yule dada alikuja kudai hela yake,’’alisema Nay.
‘’Nikatoa kama elfu tano hivi kwenye mfuko wa kushoto wa nguo yangu alikuwa akinidai elfu mbili na mia saba akaenda kutafuta chenji baadaye akarudi akanipa chenji lakini Yule dada alikuwa amesimama muda mrefu upande wa kulia kwangu akawa ananiongelesha nikamwambia siwezi kuongea naye kwakuwa naongea na simu akaniambia poa sikuzingatia sana lakini baada ya dakika mbili au tatu nikageuka sikuiona wallet yangu nikauliza kuna mtu amesogea hapa nikaambiwa hakuna mtu aliyesogea hapa,’’ aliongeza Nay.
‘’Zaidi ya Yule dada muuza juisi nikamuulizia wakaniambia amekwenda kuongeza juisi anarudi nikasema poa lakini mimi siioni wallet yangu nikatatufa kila sehemu kwenye gari sikuiona tukaanza kumfuatilia Yule dada lakini hakurudi tena’’
Aidha Nay alisema kuwa anachoshukuru pamoja na kupoteza pesa zake,siku ya pili yake alipigiwa simu kuwa vitambulisho vyake kikiwemo cha kupigia kura vimeokotwa akaenda akavichukua.

No comments: