Thursday, 3 September 2015

MWANDOSYA AMPIGA DONGO KIKWETE KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI YA MAADILI.

Prof Mark Mwandosya
BAO LA MKONO LA KIKWETE MJINI DODOMA BADO LAMSUMBUWA PROF MWANDOSYA, ETI HATA WAZIRI MKUU WA SERIKALI YA KIKWETE AU MAKAMU WA RAIS WA KIKWETE HAWAMO KWENYE TANO BORA, BASI NI SERIKALI DHAIFU!!!!!

Prof Mark Mwandosya asema :
"Mwenyekiti alikuwa na majina yake mfukoni kutoka nyumbani kwake"
Mwl J.K Nyerere aliwakataza viongozi kushaurisna na wake zao na kufanya maamuzi yanayoathiri haki za wengi lakini Kikwete amefanya hivyo kule Dodoma na hata ktk masuala mengi ya taifa hili. Kikwete ni mtu wa hila, ana roho ya inda na ni mzandiki.
Mzee Lowassa ni mtu makini, lakini Kikwete alipoona Lowassa anaikosoa serikali ya CCM, akamtuma Makonda amtukane. CCM hawajui kama Lowassa alikuwa anawatetea wananchi aliposema "viongozi wa serikali wanalalamika badala ya kutatua shida za wananchi, naomba viongozi wafanye maamuzi magumu; haiwezekani raia walalsmike na viongozi walalamike nani atatatua shida??

Lowassa alikuwa mchapakazi akashawishi maji ya ziwa Victoria yawanufaishe watanzania, akasukuma ujenzi wa shule za kata na mkakati wa chuo kikuu cha Dodoma.
Alipotaka kusitisha mkataba wa richmond ambao familia ya mkubwa ilikuwa na mkono wake akaambiwa "usithubutu hata kidogo" Watanzania kupitia Kikwete wakaingizwa mkenge kuwa ni Lowassa ndiye alishinikiza Richmond ipewe zabuni wakati hakuwepo hata katika kikao cha uteuzi wa mzabuni.
Lowassa akaendelea kusimamia haki akijua ipo siku atashika madaraka ya juu na kuuvunja mfumo mbovu ndani ya CCM hivyo kuleta mabadiliko na kurejesha haki.
Kikwete alipoona Lowassa anatakiwa na watu wengi kuwa Rais, akaamua kuizima hiyo ndoto akiwatumia vijana wake Nape, Makonda na Januari Makamba.

Profesa Mark Mwandosya anasema
'majina matano yaliyoletwa kamati kuu hayakupitia kamati ya maadili ila yalikuwa majina ya mwenyekiti kutoka mfukoni mwake''
Kwa mizengwe hiyo, haijalishi Magufuli alipitishwa na watu walionuia kumkomoa Kikwete, bado itakuwa ni kuendelea kuiunga mkono CCM na Kikwete na mizengwe yake ni kuendeleza mfumo mbovu.
Tatizo letu hatujui nini kilitokea Dodoma na tulikuja kusikia kesho yake tu kuwa Magufuli amepita tusijue mikiki mikiki iliyopelekea Magufuli kupita.
Mwandosya anasema mkutano ule ulipoa, hata mwenyekiti (Kikwete) alipoongea watu hawakumshangilia na hata Nape alipowataka wajumbe wamshangilie hawakufanya hivyo.

Maana yake nini? -> Lowassa kuondoka CCM ni kutafuta mabadiliko nje ya CCM ambayo bila shaka hayawezi kupatikana CCM kama alivyowahi kutabiri Nyerere. Hata Magufuli hawezi kuvunja mfumo huo na anatakiwa kumpigia kura Lowassa kama alivyokuwa amepanga kufanya alipoenda Dodoma kabla hajajua kama jina lake lingewekwa kama kiegesheo katika majina matatu ya Kikwete aliyoyajadili na mkewe
Mwandosya anasema Magufuli hajawahi kuwa mwenyekiti wa CCM (W) hata kijiji wala kata atamudu vipi uenyekiti wa CCM taifa na kuvunja mfumo mbovu?

Maneno ya Prof huyu yanamaanisha kuwa kuna watu wengi wataendelea kuvaa nguo ya kijani ila watampigia kura Edward Lowassa

No comments: