Monday, 19 October 2015

BREAKING NEWZ!!! KATIBU WA BUNGE APATA AJALI AKIENDA LUDEWA KUMZIKA FILIKUNJOMBE.

Katibu wa bunge amepata ajali akiwa anaelekea Ludewa{Mbeya} kumzika Marehemu Deo Filikunjombe aliyefariki kwa ajali ya Chopa katika Mbuga za Selous juzi usiku.....
Katika Ajali hii wote wametoka salama na hakuna aliyepoteza Maisha.

Gari la ziada katika msafara wa Spika wa Bunge likiwa limepinduka wakati wakiwa njiani kuelekea katika mazishi ya Marehemu Deo Filikunjombe huko Ludewa. Ajali hiyo imewahusisha Mlinzi wa Spika, Alphonse Mwakasege, Naibu Katibu wa Spika,Herman Berege na Mbunge wa Mafia anaemaliza muda wake, Mhe Abdulkarim Shah.

Abiria wote wamepata majeraha madogo madogo na waliokolewa katika eneo hilo na Mhe. William Lukuvi, Mb na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi.

Picha kwa hisani ya: Ofisi ya Bunge.

No comments: