![]() |
| Waziri Mkuu, Mizengo Pinda |
Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni jana, Pinda alisema anamshukuru Mungu kwa kumaliza salama nafasi aliyopewa ya kulitumikia taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa na katika ngazi ya uwaziri miaka miwili na nusu na miaka mitano akiwa Naibu Waziri.
“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza salama uongozi wangu serikalini. Ninamaliza uongozi wangu kwa amani na furaha. Katika ibada hii ya shukrani nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi… yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua,” alisema na kuongeza:
“Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi. Nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa Naibu Waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu.”
“Wito wangu kwa Watanzania wote ni kwamba msiache kumtanguliza Mungu maishani kwa sababu yeye ndiye mtoaji wa yote. Wote tuendelee kumtii na viongozi wetu wa kiroho kwa sababu wako hapa kumwakilisha yeye.”

No comments:
Post a Comment