Tuesday, 20 October 2015

CHADEMA WAMSHITAKI RAIS KIKWETE UMOJA WA MATAIFA{UN}

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema tayari kimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, kumshtaki Rais Jakaya Kikwete.
Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa barua hiyo waliituma UN jana.
Mallya alisema lengo la barua ni kumshtaki Rais Kikwete kwa mataifa mengine kutokana na kauli yake ya kuwatisha Watanzania aliyodai aliitoa Oktoba 14, mwaka huu ya kuwataka wapigakura kuondoka kituoni baada ya kupiga kura na endapo watakiuka watashughulikiwa.
Mallya alisema kauli ya Rais Kikwete ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi inayomtaka mpigakura kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.
Kuhusu wananchi kukaa mita 200, Mwanasheria huyo wa Chadema alisema jambo hilo ni kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1985 kifungu cha 104 inayomruhusu mpigakura kukaa nje ya mita hizo.
Akizungumzia suala la kuhamasisha amani wakati huu wa kuelekea kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo, Mallya alisema chama hicho kinahubiri amani, lakini hakiwezi kukaa kimya endapo kutakuwapo uvunjifu wa sheria.

No comments: