Tuesday, 6 October 2015

MAGUFULI AMFAGILIA Dr,SLAA.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli jana jioni alihutubia katika Jimbo la Karatu Mkoani Arusha

-Alisema aliyekuwa Katibu wa CHADEMA, Dr. Slaa ni kiongozi mwenye msimamo.


Alianza utangulizi Lekule Laizer ambae mbunge Longido na kumkaribisha mwenyekiti wa wazazi ambae nae akamkaribisha mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi.

Magufuli ameanza kuhutubia na anaomba radhi kwa kuchelewa kwani wamesimamishwa sana njiani kwa watu kuwazuia ili wasalimie na wasingeweza kuwapita kibinaadamu.

Ndugu Wilbroad Slaa mimi namfagilia sana, tunataka viongozi wenye msimamo ndio maana namfagilia hata kama hayuko CCM. Mimi sikuja hapa kuomba kura kwa sababu nataka kuwa Rais wa chama kimoja bali Rais wa watu wote.

Nimeshazungumza serikali ya awamu ya tano, tutahakikisha tunajenga mahusiano mazuri na wanaoishi kandokando na maeneo ya utalii, Karatu wananchi wako wengi wanaojitahidi kujitengenezea maisha yao lakini imekuwa ni tatizo.

Nimekaa serikali miaka 20 sijawahi kufukuzwa, nimekuwa mbunge miaka 20 na miaka kumi nimepitwa bila kupingwa. Ninachokisema ninakiamini na kipo moyoni mwangu, jukumu langu kubwa itakuwa ni kuwafanyia kazi.


Nataka niwahakikishie mimi ndio kiboko ya mafisadi, wale wabaya wameanza kukimbia. Mke wangu ni mwalimu wa shule ya msingi mpaka leo, nayafahamu magumu wanayoyaishi, nataka makato ya asilimia 11 tuyashushe.


NB:-Iangalie VIDEO ya Mkutano huo hapo chini..... 

No comments: