hamjambo
ndugu zangu? Poleni na shughuli za kila siku? kuna story ya abiria wa
treni ya reli ya kati walokuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es Salaam
kwenda Morogoro,Dodoma,Kigoma ,Mwanza na maeneo mengine na kutelekezwa
katika eneo la pugu kwa saa 16 na shirika la reli Tanzania niliyoitoa
jana kupitia Itv, imesababisha kupigiwa simu na watu wawili ambao
hawakutaka kutaja majina yao na kunitishia kwamba watanifundisha adabu
kutokana na kuripoti habari hiyo huku wakihoji eti kwanini
nilitoa habari hiyo kwenye Itv wakati vyombo vingine vya habari
hawakuripoti story hiyo? Licha ya kujitetea kwamba siwezi kuacha kufanya
habari yeyote eti kwasababu vyombo vingine vya habari haviripoti habari
hiyo hawakutaka kunisikiliza zaidi ya kuongeza vitisho dhidi yangu.
Sasa ninachojiuliza hivi kwa hali ya abiria walivyokuwa wametelekezwa na
kuachwa ktk eneo ambalo hakuna huduma za kijamii huku baadhi ya
mabehewa kujaa wadudu na baadhi watoto, wazee na wagonjwa wakiwa katika
hali mbaya ni sawa? Hivi sisi wanahabari tusipoonyesha haya nani
ataonyesha ili jamii iweze kujua namna ambavyo shirika la reli
isivyojali wateja wake? Licha ya kutoa taarifa polisi kutokana na
vitisho hivyo na nimewasilisha namba za simu walizotimia kunipigia
lakini mimi binafsi kama SamMahela nikiwa nawakilisha Itv sitaacha
kuripoti au kuandika habari yeyote eti kwa kuogopa kuuwawa au kwa
kutishwa na mtu awaye yeyote eti kwa kufanya hivyo tutawaharibia baadhi
ya watu katika nafasi zao. Nitaendelea kufanya kazi zangu kwa mujibu wa
sheria na utaratibu wa kampuni niliyoajiriwa na kwa kuwa MUNGU amenipa
nafasi hii nitajitahidi kusimama katika nafasi yangu nikiwa bado hai
bila uwoga wowote ili siku maisha yangu yakimalizika hapa duniani basi
nami nije niende mbele zake nikisena nilitumia nafasi yangu kutetea
watu,kusaidia wahitaji na hata kutumia nafasi yangu kufichua mambo,
nadhani itakuwa jambo njema kuliko kutoripoti habari kama ile eti kwa
kuogopa kutishwa. Nimeona niwashirikishe hili na MWENYEZI MUNGU
anisimamie mie mwanae......Amina
1 comment:
Be strong bro u gat 2 keep on moving God be with u
Post a Comment