![]() |
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye |
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa
njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa
Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la
gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na
kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
![]() |
Muonekano wa gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, Toyota Land Cruiser baada ya kupata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam. |
![]() |
Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo. |
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake
na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo
ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu, Nape
amesema: “Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe
na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa,
nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.
![]() |
Muonekano wa Gari hilo kwa mbele. |
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia.”
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini
Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk.
John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji
la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na
kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
No comments:
Post a Comment