Bingwa wa Olimpiki wa mbio za
walemavu Oscar Pistorius, ataachiliwa huru kutoka gerezani Jumanne ya
wiki ijayo na kutumikia kifungo chake nyumbani baada ya bodi ya Msamaha nchini humo kutoa msamaha
kwa wafungwa Afrika kusini.
Pistorius alifungwa jela miaka mitano mwaka 2014 baada ya kupatikana
na kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia.Upande wa mashtaka umekata rufaa ukisema alifaa kuhukumiwa kwa mauaji, Rufaa hiyo itasikizwa Novemba 3 na iwapo atakutwa na hatia kifungo kinaweza ongezwa na kuwa miaka 15.
Pistorius amekaa jela miezi 12 na sasa atatumikia kipindi kilichosalia cha kifungo chake chini ya “uangalizi wa maafisa wa magereza,” bodi hiyo ya msamaha imesema.
Uamuzi wa awali wa kumwachilia huru Agosti ulisimamishwa na Waziri wa Haki wa Afrika Kusini Michael Masutha, aliyesema uamuzi huo ulikuwa umefanywa “mapema mno”.
No comments:
Post a Comment