![]() |
| Destiny’s child |
Mathew Knowles anayesimamia kundi hilo amesisitiza kuwa mipango inaendelea kwa wasichana hao wakiongozwa na Beyonce, Michelle williams na Kelly Rowland kuingia studio na kurekodi Album mpya.
Mathew Knowles aliyewahi pia kuwa meneja wa Beyonce alifukuzwa kazi na binti yake mwaka 2011 aliliambia jarida la Heat kuwa alipokea email kutoka kwa Michelle williams aliyedai kuwa alikua tayari kuungana na wenzake kwa ajili ya kurekodi Album mpya.
Tetesi za ujio wa Album mpya ya kundi la Destiny’s child zilianza kusika mwanzoni mwa mwaka huu.


No comments:
Post a Comment