![]() |
| Mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA Bw,Tumaini Makene. |
Polisi jijini jana usiku walivamia kituo cha kukusanyia matokeo ya Nchi nzima cha CHADEMA kilichopo Kijitonyama na kuwakamata watu wote wanaokiendesha.
Mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene alisema tukio hilo lilitokea saa Nne Usiku wakati vijana hao wakiendelea kukusanya matokeo hayo.
Alisema kituo hicho ambacho kulikuwa kikiendeshwa na vijana 800 na wengine maelfu walioko mikoani,kilianza kazi hiyo jana asubuhi kikilenga kukusanya matokeo yote kabla matokeo ya jumla kutangazwa na NEC.
Kamanda wa polisi Wilaya ya Kinondoni, Camillius Wambura alisema kwa sasa polisi wapo kwenye oparesheni nyingi na watu mbalimbali wanakamatwa,hivyo asingeweza jua kama watu hao wapo kwenye hiyo oparesheni.
Chanzo-Times Fm

No comments:
Post a Comment