Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania D.k Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Mamlaka ya Ustawi Makao Makuu CDA kuhakikisha mji wa Dodoma unajengwa kwa mpangilio ili kuleta taswira nzuri zaidi ya mji huo.
Akizungumza jana mara baada ya kuzindua jengo la Hazina ndogo, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Seriakali ( CAG )na jengo la Benki kuu ya Tanzania ( BOT ) kanda ya kati yaliyopo katika barabara ya kuelekea chuo kikuu cha Dododma UDOM, Rais Kikwete amesema eneo hilo lote kuelekea UDOM linapaswa kuwa na majengo yenye mueonekano unaoendana na majengo hayo.
Amesema ujenzi wa majengo hayo matatu katika mkoa wa Dodoma, ndiyo safari ya makao makuu kuhamia Dodoma hivyo CDA wanapaswa kuhakisha eneo hilo linapangwa vizuri. Aidha ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka mazingira ya ofisi hizo tatu katika hali ya usafi tofauti na ilivyo sasa huku akiwataka watumishi wa ofisi hizo kufanya kazi kwa bidii kwani bila hivyo hakutakuwa na maana ya kuwepo kwa majengo hayo.

No comments:
Post a Comment