Tuesday, 20 October 2015

RUNGWE ATOA KALI AAHAIDI KUANZISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUTUMIA HELIKOPTA NA NDEGE.

Mgombea urais kupitia chama cha ukombozi wa uma– CHAUMA Hashim Rungwe.

Mh.Rungwe aahidi kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kitafanywa na helkopta na ndege.
Mgombea urais kupitia chama cha ukombozi wa uma– CHAUMA Hashim Rungwe amesema, akichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu ujao, atahakikisha kilimo cha umwagiliaji kitafanywa na helkopta na ndege, ili kuongeza uzalishaji wa mazao katika kukabiliana na tishio la njaa nchini.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya mkuti wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mheshimiwa Rungwe amesema, inasikitisha kuona taifa baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhuru, wananchi wake wamekuwa wakikabiliwa mara kwa mara na njaa kutokana na kilimo cha kutegemea mvua, huku nchi ikiwa na mabonde mengi mazuri kwa kilimo, na hivyo akasisitiza, akichaguliwa kuwa rais wa serikali ya awamu ya 5, atahakikisha kilimo cha umwagiliaji kitafanywa na helkopta na ndege, ili taifa lijitosheleze kwa chakula.
Aidha kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Rungwe aliwauliza wananchi kama watamchagua kuwa rais wao, nao walimwitikia kuwa watamchagua, ambapo alidai yeye anafaa kuchaguliwa kuwa rais, kwa kuwa sio mwizi au fisadi, na kuongeza, moja kazi atakayofanya akichaguliwa, ni kuimarisha kitengo cha uanasheria, ili wananchi wenye matatizo ya kisheria, waweze kusaidiwa.

No comments: