Tuesday, 20 October 2015

WAZEE WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WASHINDWA KUTOFAUTISHA WAGOMBEA WATAKAOGOMBEA UCHAGUZI MKUU 2015.


Yabainika wazee na wasiojua kusoma na kuandika washindwa kutofautisha picha za wagombea Vijijini. 

Wakati muda wa uchaguzi ukielekea ukingoni baadhi ya wazee na watu wasiojua kusoma na kuandika hasa wa maeneo ya vijijini wamebainika kushindwa kutofautisha picha za wagombea urais, ubunge na udiwani zilizoko kwenye karatasi za kura jambo linaloweza kuwasababishia washindwe kuwachangua viongozi wanaowatarajia.
Tatizo hilo limebainishwa na baadhi ya wagombea udiwani wa vyama vinavyounda (UKAWA) ambao wamesema pamoja na kutumia muda mwingi kuwaelimisha tatizo hilo ni kubwa na elimu zaidi inahitajika na wameendelea kuwaomba watanzania kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko kwa kumchagua Mh.Lowassa kwani ndiye mwenye uwezo wa kumaliza matatizo hayo.
Wananchi wanakabiliwa na tatizo la kutokujua kusoma na kuandika wamesema limekuwa likiwasababishia kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo,kukosa,haki zao za msingi na kushindwa kutunza siri zao.
Wakiwa katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima mwanzoni mwa wiki viongozi wa idara ya elimu mkoa wa Arusha wamesema wanaendelea kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika kupitia mpango wa kupeleka huduma ya elimu katika maeneo waliko na wanapofanyia shughuli zao.
Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika ambapo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 kati ya watu 1,694,310 wanaojua kusoma na kuandika ni 1,372,391 na wasiojua kusoma ni 321,918 takwimu ambazo hata hivyo zitakuwa zimebadilika katika kipindi hiki cha kufikia mwaka 2015.

No comments: