Saturday, 10 October 2015

TANZIA: Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo afariki dunia.

Aliyekuwa Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT WAZALENDO Marehemu Estomih Malla aliyefariki dunia juzi saa saba Usiku katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.

Sisi sote ni wa mola na hakika kwake sote tutarejea.

=========
UPDATES:


Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ameithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki usiku wa Oktoba 9, 2015 saa Saba usiku.

Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.

No comments: