Saturday, 17 October 2015

UKAWA WAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KUDAI UHALALI WA SHERIA YA KULINDA KURA MITA MIA MBILI.

Wakili Peter Kibatara.
CHADEMA imefungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania, ikitaka tafsiri sahihi ya sheria kama mpiga kura anaruhusiwa kukaa mita 200 kusubiri matokeo yatangazwe.

-Kesi hiyo imefunguliwa chini ya hati ya haraka sana.


Kulinda kura: Wakili Peter Kibatala afungua kesi Mahakama Kuu

Tayari wakili jembe na nguli Peter Kibatala akiambatana na wanasheria nguli wa Ukawa Prof Safari, Mallya na Tundu Lissu asubuhi ya leo amefungua kesi mahakama kuu kuishitaki NEC kwa ukiukwaji wa sheria juu ya wananchi kukaa mita mia mbili na kulinda kura.

Kesi imefunguliwa under certificate of urgency nadhani kama sijakosea kwa kiswahili ni 'hati ya dharura' ili isikilizwe na tafsiri itoke kabla ya uchaguzi.Tayari jalada lishapelekwa kwa pilato na wanasheria nguli wa Ukawa wamejipanga kwa hoja za nguvu na ushahidi wa kutosha.

Pia jopo la wanasheria nguli wa UKAWA wameiomba mahakama kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya matamshi ya rais wa nchi kuwa alitumia mamlaka gani kuvaa kazi za tume.

Leo,16th October 2015, tumefungua Kesi chini ya hati ya haraka sana (certificate of extreme urgency) shauri nambari 37 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Main Registry) tukiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Tanzania na itamke iwapo wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meter 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho ya kura.

Tumeiomba pia Mahakama Kuu itamke iwapo ni halali kwa Rais wa nchi kutoa matamko aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura/raia wenye shauku kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meters 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho.

Pia tumeiomba Mahakama Kuu itamke iwapo Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi Tanzania.

Tunasubiri taratibu za kiMahakama kuhusu shauri tajwa
.

 

No comments: