Tuesday, 10 November 2015

ACT-Wazalendo Washauri Posho ya Vikao vya Bunge na Ziara za Kamati zifutwe.

Sitting allowance ya wabunge zifutwe na kubakia na mshahara tu! Hela ya dereva sijui msaidizi zote ziondolewe! Malipo ya vikao vya kamati zifutwe. Mfuko wa Jimbo ufutwe, Safari za Ulaya za kamati vibali kwa Rais. Wabunge walipwe mishahara tu na magari wakopeshwe. Ni maoni yangu tu ila kwakuwa Rais alikuwa Mbunge najua gharama halisi anazijua.
La mwisho ni I LOVE MY PRESIDENT! Najisikia raha kusema huyu ni Rais wangu.


Huu ndio wakati wa kuzitupulia mbali posho za wabunge (posho za kukalia kiti cha bunge) , posho hizi hazina tija zipingwe kwa nguvu zote.

Tumemuagiza mbunge wetu Mteule Zittokabwe asichukue posho, tunawaomba wabunge wote mzitupilie mbali posho zikasaidie maskini huko vijijini.

Pia tunategemea na kuamini Rais John Pombe Magufuli ukiisoma Ilani yetu utakubaliana nasi kuwa kuna umuhimu wa kuzifutilia mbali posho za Wabunge. Posho za wabunge ni sehemu mojawapo ya upendeleo na unyonyaji unaendelea nchini kwetu, huu ni wakati Wa mabadiliko sasa ukomeshwe kabisa.

Kama posho zisizokuwa na tija zitasitishwa na kukomeshwa zisiishie taasisi ya bunge tu iwe Taasisi zote zilizopo hapa nchini ili tujenge nchi yetu upya.

#PoshoSasaBasi


ACT-Wazalendo Taifa Kwanza

No comments: