Sunday, 22 November 2015

Hofu yatanda kwa viogozi wa vyama vya siasa mkoani Geita kuhusu Kifo Cha Mawazo.

Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie amesema kuna dalili za baadhi ya watu kutaka kuchafua amani iliyopo Wilayani hapo kwa kutoa taarifa zisizo na ukweli juu ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Alphonce Mawazo huku  baadhi ya watu kutishiwa maisha.
Amesema kuwa zipo taarifa za kiintelijensia na pia ushahidi wa ujumbe mfupi unaotishia kuwaua viongozi wa vyama vya siasa Wilaya na Mkoa wa Geita wakihusishwa na tukio la Kifo cha Mawazo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake amesema  kutokana na kuenea kwa taarifa zisizo rasmi kumepelekea kujengeka kwa chuki katika jamii na sasa linakaribia kuharibu hali ya ulinzi na usalama wa wananchi wengine.
Ameongeza kuwa baadhi ya watu wameenda mbali zaidi kwa kuandika katika mitandao ya kijamii kuwahamasisha wananchi kubeba zana za jadi kipindi cha kuaga mwili wa Marehemu Mawazo.
Nao wakazi wa Geita wanaona kuwa ni vyema hatua za haraka zikachukuliwa kuzuia machafuko lakini pia Jeshi la Polisi lifanye kazi ya kuhakikisha wanawakamata wahusika waliofanya tukio hilo.
 Mkuu wa Wilaya Mangochie ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya haraka uchunguzi wa matukio haya na kuhakikisha wanaweka mfumo mzuri na kufika kwenye matukio kwa haraka pindi wanapopata taarifa.

Chanzo-Star tv

No comments: