Thursday, 19 November 2015

NDUGU AUA MDOGO WAKE BAADA YA KUMKUTA AKIJAMIAANA NA NGURUWE.

Mtoto wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa mkoani Njombe Simon Dastani amefariki dunia baada ya kupigwa kwa fimbo na kaka yake baada ya kukutwa akifanya mapenzi na nguruwe. Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa kijana huyo aliuwawa baada ya kaka yake kusikia kuwa ameidhalilisha familia yao kwa kufanya mapenzi na mnyama na kuanza kumchapa kwa fimbo kitu kilicho sababisha kutoka damu nyingi na kupelekea kifo chake.

No comments: