Friday, 27 November 2015

Mahakama Kuu yampa ushindi Baba wa Mawazo, Mawazo kuagwa na kuzikwa kwa heshima zote.

Heshima mbele,

Mahakama kuu kanda ya Mwanza, kuanzia muda huu, itaanza kusoma hukumu dhidi ya kesi ya kuruhusu kukusanyika kwa ibada na kuaga mwili wa kamanda Mawazo, aliekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita.

Mwanza mvua inanyeshwa na watu wengi wameshajitokeza katika viwanja vya mahakama kuu Mwanza.

Mawakili wa upande wa mashitaka wamekwishaingia wakiongozwa na Wakili Msomi John Milya, Poul Kipeja na James Ole Millya (MB).

Mzazi wa marehemu Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko, baadhi ya wabunge wa UKAWA wameishaingia na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh.Mbowe.

Jaji nae anaeingia anaketi na muda wowote hukumu itaanza kusomwa. Kama kawaida askari wametanda kila kona za barabara za kuingia mahakama kuu kanda ya Mwanza.

Update:
Jiji Lameck Malacha anaendelea kusoma maelezo ya upande wa mashitaka..

Last Uptade:
Familia ya Kamanda Mawazo na CHADEMA wamepewa haki zote za kumuaga na kumzika marehemu. Hivyo wameshinda kesi ya msingi dhidi ya serikali.





Quote By Tumaini Makene View Post
Kesi ya msingi imemalizika kwa Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa, kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kuamua kwamba;
Agizo la Polisi la kuzuia kuagwa Kamanda Mawazo limefutwa na Mahakama Kuu.

Wafiwa wameruhusiwa na mahakama kumwaga Kamanda Mawazo kwa kujadiliana na polisi sehemu ya kuagia

Polisi watoe ulinzi kama ilivyo wajibu wao bila kuvuka mipaka ya kazi zao.

No comments: