Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora jana imewahukumu kunyongwa
hadi kufa Muheshimiwa Sakalambi na wenzake wawili waliokuwa wanakabiliwa
na mashitaka ya mauaji ya watu wawili kwa kukusudia.
Watu hao walipanga njama za kutekeleza mauaji ya watu wawili mume na mkewe julai 9/2012 kwa kuwakatakata na mapanga hadi kifo katika kijiji cha Inala one Kata Ndevelwa katika Manispaa ya Tabora.
Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa zaidi ya masaa mawili na Jaji John Utamwa amesema ameridhika pasipo shaka na ushahidi wa mazingira ulioungwa mkono na maelezo waliyotoa kwa onyo mbele ya mlinzi wa amani kukiri kuhusika na mauaji ya watu wawili mke na mume.
Kutokana na kurizika na ushahidi uliotolewa Jaji Utamwa amewahukumu kunyongwa hadi kifo Mheshimiwa Sakalambi na watu aliowatuma kwenda kutekeleza mauaji ya Dada yake Amina Ally na Shemeji yake Khalid Said kwa kuwakatakata mapanga hadi kifo ambao ni Jumanne Mohamed na Mabula Masanja .
Jaji Utamwa akichambua mwenendo mzima wa kesi hiyo amesema kuwa maelezo ya onyo ya washitakiwa hao yamekusanya mpango mzima wa utekelezaji wa mauaji hayo ambayo chanzo chake ni ugomvi wa mashamba na imani za kishirikina baina yao.
Amesema kwamba kutokuelewana kati ya mshitakiwa wa tatu aitwaye Mheshimiwa Sakalambi na Amina Ally ambaye ni dada yake na mumewe Khalid Said ambao sasa ni marehemu kulimfanya akodi watu wawili wa kumsaidi kufanya mauaji hayo ya kinyama.
Awali wakili wa serikali Idd Mgeni aliiambia mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo julai 9/2012 majira ya jioni katika kijiji cha Inala wani kata ya Ndevelwa Manispaa ya Tabora.
Wakili Mgeni ameongeza kuwa Khalid na mkewe Amina walifariki baadaye kutokana na kuvuja damu nyingi kulikosababishwa na majeraha waliyopata kwa kukatwa katwa kwa panga na wauaji hao ambao walikuwa wameaidiwa ujila wa shilingi million moja.
Washitakiwa wamewakilishwa na mawakili wasomi Kamaliza Kayaga na Timotheo Sichilima walikana mashitaka hayo na katika utetezi wao walitofautiana kwenye maelezo ambapo mmoja alidai anawafahamu wenzake huku wao wakikana hilo.
Sakalambi ambaye ni mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo alidai kwamba siku ya tukio alikuwa safarini Kibondo na alirudi usiku na kukuta majirani zake hao wameishafariki utetezi uliopingana na mashahidi wake aliowaleta kumtetea akiwemo mkewe mdogo na mtoto wake.
Chakushangaza mke mdogo wa mshitakiwa wa tatu Asha Jumanne na mwananye wa kiume waliiambia mahakama hiyo kuwa Sakalambi alikuwepo nyumbani na aliwakataza kwenda kutoa msaaada waliposikia kelele toka kwa ndugu zao.
Jaji Utamwa katika hitimisho lake amedai kuwa maelezo ya utetezi wa washitakiwa hayana nguvu bali yanataka kuwakwepesha kwenye mkono wa sheria ndipo akawahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa hao watatu huku akimwachilia huru mshitakiwa wanne Joseph Bundala.
Chanzo-Star tv

No comments:
Post a Comment