Tuesday, 10 November 2015

Mimi siyo Punda sibebi dawa za kulevya -Shilole.

Msanii wa kike wa muziki wa Bongofleva Shilole alimaarufu kama 'Shishi Baby' amefunguka na kusema habebi dawa ya kulevya kwani yeye si punda ila anapokwenda nje anakwenda kufanya kazi zake na sanaa.
Shilole alipokuwa akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, ambapo amesema watu wengi huwa wanakuwa na dhana hiyo wakidhani labda wasanii wanapokwenda nje huwa wanabeba dawa za kulevya lakini kwa upande wake amekana wazi na kusema anapenda kazi yake ya muziki na kuiheshimu hivyo huwa hafanya kazi hiyo ya kubeba dawa za kulevya.
“Siwezi kukataa ni kweli wapo watu wanakuja kunishawishi lakini namshukuru Mungu nina akili sana hivyo huwa nafikiria sana maisha ya wanangu na kuuweka ushawishi pembeni, na nikimuwaza mpenzi wangu Nuh Mziwanda naona bora hayo mambo yanipite pembeni nisije kuharibu ndoto za maisha yangu na wanangu kwa mambo kama hayo,” alisema Shilole.
Katika hatua nyingine Shilole ameelezea nia yake ya kuja kufunga ndoa na mpenzi wake huyo Nuh Mziwanda na kudai kuwa kwa sasa wanajipanga na muda ukifika watafunga ndoa maana wanataka kufanya harusi kubwa na si kukurupuka tu, kufunga ndoa ya kawaida.

Chanzo-EATV

No comments: