Saturday, 28 November 2015

MUUZA MADAWA MAARUFU MAENEO YA MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM AKAMATWA NA JESHI LA POLISI.

Madawa ya Kulevya yakiwa yamefungwa tayari kwa kusafirishwa,
Vita dhidi ya Madawa ya Kulevya: Mshukiwa wa siku nyingi, Hussein Mafisi akamatwa jijini Dar.

- Alikuwa akiuza madawa hayo eneo la Mwenge Dar, akamatwa akiwa na kundi la mateja akiwauzia.


Siku kadhaa nyuma niliweka Uzi unaosema Hussein Mafisi analindwa na nani?

Kwenye Uzi huo nililalamika ni nani anayemlinda Hussein Mafisi muuza madawa maarufu Mwenge. Leo muda wa saa 9 na dakika 45 amekamatwa. Gari tatu za Polisi zilifika Dukani kwake na kubeba mateja wote waliokuwepo na Hussein wenyewe..

Hii ni mara ya kwanza kukamatwa, daima hukamatwa mateja na yeye huachwa, lakini Leo kakamatwa. Nitasikitika Sana kama nitamkuta tena jioni akiendelea na biashara yake.  


Chanzo-Jamii Forum.

No comments: