GUMZO!
Miezi kadhaa imekatika tangu nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kumwagana na mumewe, Emmanuel Mbasha ‘Imma’, habari ya mjini kwa sasa ni mwanadada huyo kudaiwa kujiachia kila kona na jamaa anayemtambulisha kwa jina moja la Peter akisema kuwa ni mlinzi wake wa karibu, Risasi Jumamosi linatumbua jipu!
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana katika hafla mbalimbali wakitembea kama kumbikumbi hali ambayo imekuwa ikizua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo ni m’badala wa Emmanuel.
“Hivi hamna habari? Yaani tangu Flora amwagane na Mbasha, amekuwa akiongozana na Peter kila mahali, eti ndiye mtu wake wa karibu. Wamekuwa wakionekana hoteli pamoja, mara katika hafla mbalimbali. Yaani sasa hivi siyo siri, kila mtu anajua ni mtu na mwenzake,” kilisema chanzo hicho.
CHANZO CHAANIKA PICHA
Kuonesha kuwa hakibahatishi, chanzo hicho kilimtumia picha mwandishi wetu inayomuonesha Peter na Flora wakiwa katika pozi la kugusanisha vichwa vyao nyuma kukiwa na tanki la maji.
“Kama vipi ngoja nikutumie picha hii ujionee mwenyewe maana nikisema hawa watu wapo karibu sana namaanisha ukaribu haswaa,” kilisema chanzo hicho huku kikimtumia picha mwandishi wetu.
UKARIBU WAO ULIANZA ZAMANI!
Baada ya mwandishi wetu kutumiwa picha hiyo, ‘kiranja’ wa gazeti hili alivuta kumbukumbu katika makabrasha yake na kubaini kuwa, wawili hao walianza kuwa karibu kwa muda mrefu lakini ukaribu wao ulikolea zaidi wakati wa kesi ya Imma akidaiwa kumbaka shemejiye iliyokuwa ikiunguruma kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar.
RISASI LILIWAHI KUWAKUTA PAMOJA!
chanzo-GPL.

No comments:
Post a Comment