Monday, 16 November 2015

Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za mauaji ya Alphonce Mawazo.

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linawashikilia watu wanne wakihusishwa na mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwambulambo amesema pamoja na kuwakamata watuhumiwa, uchunguzi bado unaendelea kuwakamata wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama.
 

Amesema kuwa hawatasita kuchukua hatua yoyote kwenye uhalifu huu.

Taarifa zinasema kuwa waliomshambulia walitumia mapanga kumkata na wakamwacha akivuja damu nyingi zilizomsababishia umauti.

No comments: