Tuesday, 1 December 2015

DEWJI AWABURUZA RAIS WA NIGERIA NA MKE WA ZUMA-TUZO ZA FOBES{AFRICA}.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji maarufu kama MO, ameshinda tuzo ya “Mtu wa Mwaka” wa jarida maarufu la Fobes katika hafla zilizofanyika jijini, Johanesburg nchini Afrika Kusini.
Katika shindano hilo, Dewji alishindanishwa katika hatua ya mwisho na mke wa Rais wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.Wengine waliokuwamo katika shindano hilo ni pamoja na Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie, ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani na Arumna Otei wa Nigeria pia ambaye ni makamu wa Rais wa benki ya Dunia.

No comments: