Tuesday, 8 December 2015

JENGO LA GHOROFA KUMI NA SITA LILILOJENGWA CHINI YA KIWANGO KUBOMOLEWA.

Kasi ya utendaji wa Rais John Magufuli, imeibua upya sakata la ubomoaji wa jengo la ghorofa 16 ambalo serikali iliamuru libomolewe baada ya kutokidhi viwango lakini viongozi walionekana kulega lega katika utekelezaji wa agizo hilo.
Azma ya kubomolewa kwa jengo hilo lililopo mtaa wa Indira Ghand na Kisutu, kunafuatia tukio la Machi 29 mwaka 2013 baada kuporomoka kwa jengo pacha lililosababisha vifo vya watu 36, na kujeruhi wengine 18.
Hata hivyo, kazi ya kubomoa imeonekana ikisuasua kwa miaka mitatu kutokana na wakandarasi wanaopewa kazi hiyo kujitoa katika hatua ya mwisho wakitoa sababu mbalimbali.
Manispaa ya Ilala sasa imetangaza kufanya kazi hiyo haraka na tayari kampuni tatu za kimataifa zimejitokeza kufanya kazi hiyo.
Akizungumza Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, David Langa alisema Halmashauri hiyo ipo katika hatua ya mwisho ya kumpata mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Alisema mpaka sasa katika zabuni iliyotangazwa kuna kampuni tatu zilizojitokeza kutaka kazi hiyo na wako katika hatua za mwisho mwisho kumpata mshidi wa zabuni hiyo.

No comments: