Jumla ya watu. 12 wamepoteza Maisha na 22 wamejeruhiwa leo baada ya
basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo.
Wanane ni wanaume na wanne ni wanawake. Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni
ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka
Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba
T616DEF katika kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika
barabara kuu ya Dar - Mbeya.
majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini.
majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini.

No comments:
Post a Comment