Thursday, 3 December 2015

MFUASI MTOTO WA BOKO HARAMU{11} AKAMATWA.

Jeshi la Nigeria linamshikilia mtoto mwenye umri wa miaka 11 aitwae Abou Usman, kwa kuhusika na shambulio liliotokea mjini Maiduguri jimbo la Borno siku kadhaa zilizopita.
Akiongea na waandishi wa Habari jana, afisa uhusiano wa jeshi hilo bwana Sani Usman amesema mtoto huyo kakiri kuhusika na shambulio hilo.
Taarifa za awali zinadai kuwa, mtoto huyo alianza kupokea mafunzo ya kijeshi tangu alipokuwa na umri wa miaka 6.
Hii si mara ya kwanza kwa jeshi hilo kukamata watoto wadogo wenye mafunzo ya kijeshi, kwani mpaka sasa wanashikilia zaidi ya watoto 26.

No comments: