Thursday, 3 December 2015

Uongozi Wilaya ya Kinondoni waagiza kiwanda cha Urafiki kifungwe.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameagiza kiwanda cha urafiki kisitishe uzalishaji na tayari kimefungwa muda huu baada ya uongozi wa kiwanda hicho kushindwa kutimiza madai ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kama ambavyo walikubaliana.

Itakumbukwa wiki iliyopita Makonda alilazimika kwenda kutuliza mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki baada ya wafanyakazi hao kuwa na madai mbalimbali kwa kipindi kirefu bila ya uongozi wa kiwanda hicho kufanyia kazi madai yao.

Aidha, wiki iliyopita baada ya DC Makonda kutinga katika mgomo huo ndipo uongozi wa kiwanda uliahidi kutimiza madai ya wafanyakazi hao Disemba 1, ijapokuwa hadi sasa kinyume na makubaliano hayo hakuna kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho.

No comments: