Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amekutana na Baraza la Sekta Binafsi leo Ikulu Jijini Dar.
Katika mkutano huo, Magufuli ametoa siku saba, kuanzia leo kwa wafanyabiashara wote walioingiza bidhaa nchini bila kulipa ushuru wakajisalimishe na kulipa.
Mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi wa Tanzania Private Sector Foundation wakiongozwa na Mwenyekiti Dk. Reginald Mengi, CEOs Round Table wakiongozwa na Mwenyekiti, Ali Mfuruki na baraza la biashara Taifa, TNBC.
Hatua hiyo imekuja kufuatia hatua kali zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa.
Hivi karibuni Magufuli alimsimamisha kazi kamishna mkuu wa TRA, Rished Bade kufuatia kupotea kwa makontena zaidi ya 300 kwenye bandari ya Dar es Salaam

No comments:
Post a Comment