Thursday, 3 December 2015

Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya Bandari tena, makontena zaidi ya 2,000 yamepita bila kodi.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa yupo ndani ya Yard za Bandari ya Dar Es Salaam katika ziara ya kushtukiza.

Alivofika Bandarini hakuingia hata katika ofisi za Meneja wa Bandari aliomba waonane sehemu ambapo wanaandika Bill of lading na baada hapo PM na alielekea eneo la Scanner. Sijui leo atatoka na nini??? #Tanzania4Change


=======================
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.

Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.

No comments: