Tuesday, 8 March 2016

Naibu Spika,Tulia Ackson awataja washindi wa Tuzo za Malkia Wa Nguvu.

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tulia Ackson leo kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds Tv na Power Breakfast cha Clouds FM.
Malkia wa Nguvu ni mwanamke ambaye tayari sii tu jamii inamtambua, bali hata yeye binafsi anajitambua, ana nafasi, na nguvu dhidi ya anachopaswa kukitafuta na kuendelea kuzitumia fursa zilizomzunguka.
Hawa ndiyo washindi wa Tuzo Za Malkia Wa Nguvu:

SHEKHA NASSER:
Ni mwanamke wa shoka, ambaye kwa kutambua thamani ya urembo katika jamii , ameamua kuanzisha Kampuni ya urembo inayofahamika kwa jina la Shear Illusions.
Shear Illusions ni Kampuni ya urembo iliyoanzishwa mwaka 2005 nchini, na ni Kampuni ambayo inajumuisha vipodozi mbalimblai kwa jumla na rejareja.
Alianzisha kampuni inayohusika na nywele na vipodozi kupitia nembo ya bidhaa yake ya Luvtouch Manjano ambavyo vyote kwa pamoja vinatoa huduma ya urembo kwa watu wa rika zote, wenye vipato vya chini na watu mashuhuri.
Kwa sasa anamiliki matawi manne ya Shear Illussions, kunakowawezesha pia vijana wengi kupata ajira.
Kwetu sisi,ni Malkia wa nguvu , kutokana na mchango wake mkubwa kwenye sekta ya urembo, na namna ambavyo ameweza kuwagusa watu wa aina zote kwa kuzingatia hali zao kiuchumi.


KHADIJA ALLY SAID
Ni mmiliki na mwanzilishi wa kampuni inayokua kwa kasi ya Haiba ya Afrika Ltd, watengenezaji na wauzaji wa asali ya bibi,ni mwanamke ambae amethibitisha uwezo wake wa kufanya shughuli anuai kwa muda mrefu na kwa umakini wa hali ya juu katika biashara zake.
Hakuna mafanikio yanayoota kama uyoga, hii inadhihirisha wazi jinsi safari ya mafanikio ya Khadija ilivyokuwa.
Safari yake ilianza mbali kidogo, alianza kama mwanaharakati wa masuala ya watoto na vijana na amini kipindi hicho harakati hizo zilikuwa kwenye vuguvugu la hakiza watoto zilikua zimeanza na kwa mara ya kwanza alishiriki mkutano maalum wa umoja wa mataifa uliojadili masuala ya haki za watoto yaaani UNGASS.
Licha ya kuwa na elimu ya juu, kiu ya hadija ya kufanya biashara
Ilianza pindi alipokua akichukua elimu yake ya juu mwaka 2006, ambapo alianzisha kampuni yake aliyopa jina la Aljazeera café inayo fanya vizuri hivi sasa.
Kampuni hii inajishughulisha na huduma za stationery, wakala wa bima na huduma za uwakala mkubwa wa mpesa na kwa sasa wakala mkubwa wa halotel.
Wewe ni malkia wetu wa nguvu kwani Miaka michache baadae ameweza kukua kibiashara na kumiliki kampuni tatu tofauti ikiwemo Ruby Real Estae company ambayo inamiliki Ruby Villas Kibada Kigamboni Dar es salaam.
Khadija ameonyesha ubora wa akili,ubunifu na uchapakazi wa mwanamke katika ngazi tofauti.
Hadija anajicho la kuona fursa za uwekezaji na hachelei kuwekeza na kuikimbiza fursa kwa mafanikio na ni msimamizi mzuri wa miradi yake.


JACQUELINE KIPANGULA
Ana miaka 24 tu, mwenyeji wa mkoa wa Iringa na mbunifu wa vitu mbalimbali vya elektroniki. Kipangula alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuchukua Shahada ya Umeme na Mawasiliano ambayo amehitimu mwaka 2014. Ubunifu wa kwanza kuuonyesha akiwa chuoni ilikuwa kutengeneza mashine inayomwagilia kwa kupima wingi wa maji kwenye udongo, inamwagilia yenyewe na kutuma taarifa kwa mwenye shamba. Kwa sasa yupo tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kama fabrication laboratory manager katika program ya BUNI.


JUDITH ZACHWA
Ni malkia wa nguvu katika sekta ya retail, akiwa na umri mdogo kabisa alitoka masomoni nje ya nchi Tanzania, na aliporudi hakuja na hela bali aliziona fursa katika sekta ya uwakala na usambazaji wa vinywaji. Katika hali ya kudunduliza na uchanga wake katika hii sekta hakukata tamaa bali aliendelea na biashara yake hiyo. Leo hii malkia huyu ni msambazaji mkubwa na anaeaminika na kampuni ya SBL Tanzania, haswa miji ya Dar es salaam na Bukoba.


YASINTA NYUYEKO
Maumivu wakati wa hedhi ni Changamoto anazozipata mwanamke kila mwezi, japo maumivu hayo hutofautina.
Kwa kuiona changamoto hiyo, mjasiriamali huyo akaona kuna umuhimu wa kumtafutia ahueni mwanamke, kwa kuja na wazo la kutengeneza taulo za kike.
Malkia huyu wa nguvu akaona kwanini asiyahamishie matumizi ya mkaa wa mianzi kwenye taulo hizo, kwani mkaa huo una madini zaidi ya 400, yakiwemo Calcium, Potasium na Magnesium ambayo mwanamke anayapoteza kwa wingi wakati wa hedhi, na upotezaji wa madini hayo bila jitihada zozote za kuyarudisha ndio chanzo cha matatizo.
Hatimaye taulo hizo za kike zijulikanazo kama Glory Girl Pad zikatambulishwa na kuanza kutumika na kujizolea sifa lukuki kwa wanawake waliozitumia kutokana na zilivyotengenezwa.
Alihakikisha hakurupuki, kwani taulo hizo zimethibitishwa na mamlaka zote zinazohusika kwa matumizi ya binaadamu baada ya kufanyiwa utafiti na kuthibitika zinafaa.
Mbali na kusambaza taulo hizo za kike nchini, alipata ofa ya kuzisambaza katika nchi za Finland na Urusi. Hakika haya ni mafanikio makubwa.
Tanzania ina kila sababu ya kujivunia malkia huyu wa nguvu kwa jitihada zake dhidi ya wanawake wenzake.

 LATIFA RASIMSI MARIMAI
Ni malkia wa mwisho katika familia yao ya watoto wane, aliesomea masomo ya Micro-Biology na kutunukiwa shahada yake ya kwanza mwaka 2014. Baada ya kumaliza masomo yake, alijikuta ni mmoja wa vijana waliokumbwa na changamoto kubwa ya kutopata ajira, kulikomfanya aanze kujiuliza ni nini cha kufanya badala ya kubweteka au kukata tama kabisa ya kujikwamua kimaisha. Hakuna asiefahamu adha ya mrundikano wa takataka hasa katika majiji makubwa likiwemo la Dar es salaam, na ndipo malkia wa nguvu LATIFA akaona aitumie fursa hiyo ili kuweka hali ya usafi jijini Dar es salaam, kupitia kampuni aliyoianzisha iliyojikita huko Gongo la Mboto, iitwayo GUAVAY COMPANY LIMITED. Kampuni hii iliyoanza kazi rasmi mwaka 2015 kwa ushirikiano wa zaidi ya mtu mmoja, inaozesha taka za majumbani na sokoni kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha taka hizo haziendelei kuwa kero kila kukicha.


MAMA ROSE ROMANUS
Alianza biashara Desemba mwaka 2009 kwa kufungua duka la vyakula la rejareja. Akiwa na mfanyakazi mmoja na chumbakimoja cha kufanyiakazi.
Mwaka 2010 alianza kununua mchele na kuufunga kisha kusambaza maofisini.
Mwaka 2011 mchele ukawa adimu nakupanda bei na hivyo kumsababishia hasara kubwa hatua iliyomfanya aachane na biashara hiyo na kujiunga na mafunzo ya usindikaji wa vyakula SIDO.
Mafunzo hayo yalimuinua mama Rose kwani baada ya kuhitimu alianza kutengeneza ungamchanganyiko (lishe) kilo 12, na soko lake likawa majirani zake.


JENNIFER BASH
Ni dada aliyefanikiwa kumiliki kampuni ijulikanayo kama AKTZ Industries Ltd. Ambayo aliisajili mwaka 2011, na Ikaanza  kazi rasmi mwaka 2012. Hii ni Kampuni iliyojikita kwenye biashara ya vyakula vinavyo zalishwa na wakulima na wafugaji wa ki Tanzania.
Pia kampuni hiyo ina fungasha bidhaa hizo kwenye vi fungashio vilivyo thibitishwa na TFDA na baada ya hapo bidhaa hizo zinapelekwa sokoni.
AKTZ imesaidia sana wakulima kupata masoko ya bidhaa zao tofauti nahapo awali. Kwa sasa kampuni  ina bidhaa tatu sokoni, Mchele, Mayai na mafuta ya alizeti vyote vinauzwa chini ya brand ya Alaska Tanzania.
Jennifer Bash anawashauri wanawake hasa wale wanaotaka kuwa wajasiriamali kwamba, Kwanza kabisa lazima utambue nini unapenda kwa upande wa biashara, fanya utafiti wa soko na uhitaji wa  hicho kitu unachopenda na  huo ndio utakua mwanzo wa safari yako ya ujasirimali ila pia unatakiwa kuangalia pande tofauti tofauti za biashara usijiwekee mipaka.
Lakini kubwa zaidi Jennifer anawataka wanawake wapendane na kujifunza kuinuana na mwanamke Alie juu ampe mkono alie chini.

FLAVIANA MATATA
Ni binti wa Kitanzania na mwanamitindo alizaliwa tarehe 9 June mnamo mwaka 1988 akiwa na elimu ya ufundi umeme alianza safari yake ya uanamitindo baada ya kushiriki mashindano ya Miss Universe Tanzania yaliofanyika mwaka 2007
Flaviana Matata ameweza kuipeperusha bendra ya Tanzania vyema katika ulimwengu wa mitindo ya mavazi, ambapo mwanamitindo huyu wa Kitanzania ameweza kutokeza kwenye kazi za mataifa mbalimbali kama Ufaransa, U.K, Hispania na Marekani anakoishi sasa huko New York na kufanya vizuri zaidi.
Flaviana ni malkia wa nguvu ambae hakutaka kuishia katika uwanamitindo pekee bali akakumbuka alikotoka na kuja na taasisi alioipa jina la Flaviana Matata foundation ambayo aliianzisha mwaka 2011 ikiwa na lengo la kuwasaidia watoto wa wenye uhitaji na watoto wa kike pia kufikia ndoto zao za kupata elimu bora kwa kuwawezesha kupata vifa avya shule kama madaftari, kalamu , viatu na hata mabegi ya kubebea vitabu vya shule.
Kwa kuanza tu kazi hizo za kusaidia jamii tumu yake ilijikita katika shule za msingi Mtua huko Nachingwea na Litingi ambapo  Wanafunzi zaidi ya 700 wa shule hizo wakapokea vifaa vya shule kutoka Flaviana Matata foundation.
Flaviana Matata foundation pia imekuwa aikifanya kazi maeneo mbalimbali nchini kama Bagamoyo na sehemu nyingine kwenye project za FMF back to school project.
Malkia huyu wa nguvu hakuishia hapo ambapo baada ya kutambua fursa ya kibiashara katika tasnia ya urembo amekuja na bidhaa yake mpya ya Lavvy Nails Polish.

ANISA MPUNGWE

Ni miongoni mwa wabunifu wachache wakitanzania wanaofanya vizuri nchi za nje kupitia kazi yao za ubunifu.Anisa mpungwe ni binti wa kitanzania anaeishi nchini afrika ya kusini ambae ameweza kujizolea umaarufu mkubwa ulioweza kumfikisha kushiriki maonyesho mbalimbali ndani na nje ya afrika kusini.

 

NASREEM KAREEM

Akiwa na miaka 22 tu alichaguliwa kuwa Miss Tanzania mwaka 2008 kwa kuwabwaga warembo wenzake wapatao 26 kutoka mikoa yote ya tanzania bara.

Mfahamu kwa jina la Nasreem Karim kwetu huyu ni malkia wa nguvu ambae ameweza kutambua na kuiiiona fursa ya bidhaa urembo wa asili kwa kufungua duka lake la bidhaa za urembo wa asili ambazo zinatengezezwa na kina mama wa kimasai linalojulikana kw ajina la ENJIPAI.

 

MILLEN MAGESE..Miss Tanzania 2001, Super Model, balozi wa elimu ya endemetriosis
Kwa mara ya kwanza watanzania wengi kulisikia neno Endometriosis, lilikuwa jina geni lililoendelea kukua kwa kasi kadri lilivyoendelea kufafanuliwa kama tatizo linalowakumba wanawake wengi na wakati mwingine bila kujitambua.
Malkia wa nguvu, miss Tanzania mwaka 2001, super model kwenye Fashion duniani, MILLEN MAGESE, ni mmoja wa wahanga wakubwa wa tatizo hilo lakini pamoja na kuwa nalo, halimzuii kutimiza ndoto zake nyingine. Tena, anashauri kutafuta msaada wa kidaktari mapema, pindi utakapoanza kuona dalili za ugonjwa huo.
Chanzo-CLOUDS MEDIA.

No comments: