Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, na mbunge
wa jimbo la Namtumbo, Eng. Edwin Ngonyani, alipiga magoti kuashiria
heshima ya kuwashukuru wananchi wake, kwa kumpigia kura nyingi zilizompa
ushindi wa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Ngonyani alipiga magoti hayo wakati akiongea na wananchi wa katika kata za Lusewa, Ligera, Luegu na kijiji cha Kilimasera wakati akiwa katika ziarya kukagua barabara pamoja na kuongea na wananchi na kusikiliza kero zao ambapo katika harakati za kuonesha heshima kwa wananchi kwa kumpa dhamana ya kuwa mtumishi wao aliamua apige magoti katika mikutano yake hiyo.
Alisema wakati anaomba kura alipiga magoti kuwaomba wapiga kura ili wamchague hivyo ni vyema pia ashukuru kwa kupiga magoti kama mwanzo alisisitiza mbunge huyo.
Mbunge huyo ambaye katika ziara hiyo aliambatana na Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Ruvuma,wakuu wa idara katika halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa lengo la kujibu hoja za wananchi kwa kuwa wao ndio wataalamu wa kutoa maelekezo kwa wananchi kutekeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali .
Katika ziara hiyo wananchi walilalamikia zaidi upatikanaji wa maji ambapo pamoja na mambo mengine walisema kuwa swala la upatikanaji wa maji limekuwa tatizo kwa kuwa visima vyote vilivyochimbwa na halmashauri ya wilaya katika baadhi ya vijiji vimeharibika na visima vingine kuibiwa pampu na kuwafanya wananchi hao kutumia maji ya mito au maji ya visima vya asili vya kuchimba kwa mkono.
Akijibu Kero hizo kwa nyakati tofauto Mhandisi wa idara ya maji wa wilaya ya Namtumbo Bakari Mwanyiro alisema kuwa miundo mbinu ya maji inayotumika hivi sasa ni ile ya zamani licha ya kuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya watumia maji na ongezeko kubwa la watu la hivi sasa.
Hata hivyo Mhandisi Mwanyiro aliilalamikia upangaji wa bajeti ndogo ya maji kuwa ndio kikwazo ikilinganishwa na mahitaji ya maji ambayo ni makubwa na kuifanya idara ya maji kulalamikiwa na wananchi na kuwafanya watumishi wa halmashauri kulalamikiwa kila kona ya halmashauri kutokana na kupewa bajeti ndogo ukilinganisha na mahitaji ya maji katika jamii

No comments:
Post a Comment