Thursday, 3 March 2016

Rais Magufuli atumia Kikwete salamu za rambirambi

Mzee Selemani Mrisho Kikwete enzi za uhai wake
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, kifo hicho kimetokea leo asubuhi nchini India.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mzee Selemani Mrisho Kikwete alikuwa nchini India kwa matibabu.
Katika salamu zake Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Mzee Selemani Mrisho Kikwete na amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete kuombeleza kifo cha mtu muhimu kwa familia hiyo.
"Napenda kukupa pole nyingi wewe Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, familia yenu yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika familia, natambua uchungu mkubwa mlionao lakini nawaomba muwe na uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu" Alisema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amemuombea Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Chanzo-EATV

No comments: