Kwa mujibu wa mmoja kati mameneja wake, ni kwamba Icon wa muziki Afrika Mashariki Naseeb ‘Diamond’ Abdul anatarajiwa kufanya Surprise kwa mashabiki wake kabla ya kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mkubwa Fella ambaye pia ni meneja wa Yamoto Band, ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna kitu Diamond atawapa wadau na mashabiki zake wiki ijayo na ni kama salam tu ya mwezi wa Ramadhan. “Chibu dangote daimond platnam jumamosi kapige kazi mwanza na inabidi na uibebe east Africa yetu Bara letu kwani anae kuja nae ni nguli na mashabiki wanataka burudani na wewe unaweza kuwatosheza mashabiki wetu wa MWANZA namie najua nini unafanya kwenye taifa ili na kuanzia weeky ijayo Kuna kitu mashabiki wako na wadau wako unataka kuwapa Salam kabla atujaanza kufunga ramadhan sasa mie naomba tuombe MUNGU atupe afya njema uje kutangazia umma na taifa kwa ujumla. ila naomba mashabiki wa mziki wetu wa mkoa ya Kanda ya ziwa #jembeka katuletea festival naomba tumpe sapot ” Ameandika Fela.

No comments:
Post a Comment