Friday, 20 May 2016

Ne-Yo atua Dar kwa kishindo, kufunika kesho Mwanza.

Staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo (katikati) akielekea kwenye gari baada ya kuwasili Dar.

Muimbaji huyo wa ‘Miss Independent’ alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mida ya saa tano kasoro usiku. Staa huyo aliyekuwa amevaa nguo zote nyeusi na kofia ambayo alikuwa ameifunika na hood aliwapungia mkono waandishi wa habari na mashabiki waliokuwa wamejitokeza kumpokea kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye gari na kufunga vioo. Mlinzi wake pandikizi la mtu, alimzuia staa huyo kutoongea na waandishi wa habari kwa kudai kuwa alihitaji kupumzika kutokana na uchovu wa safari hiyo. Hata hivyo baada ya kuombwa na waandishi wa habari walau wamuulize maswali machache, alifungua kioo cha gari na Ne-Yo kusalimia. “Fantastic so far,” alijibu Ne-Yo baada ya kuulizwa anajisikiaje kuja Tanzania. “ I am happy to be here looking forward to perform with Diamond and everyone who will be at the show,” aliongeza. Ne-Yo atatumbuiza Jumamosi hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka linalodhaminiwa na Vodacom. Diamond na wasanii wengine zaidi ya 20 watatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM. Baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Ne-Yo alienda kwenye hafla ya Meet and Greet iliyofanyika Club Rouge iliyopo kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Warembo na wapenzi wa burudani wakimsubiri Ne-Yo.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom, Matina Nkurlu akiongea na wanahabari.

Wanahabari na baadhi ya mashabiki wakati wakimsubiri staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo usiku wa kuamkia leo.

 STAA wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo ametua usiku wa kuamkia leo ambapo anatarajiwa kupiga bonge la shoo kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Ne-Yo anayebamba na vibao vikali kama Because of You, Miss Independent na vingine vingi, alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mida ya saa tano akiwa ameambatana na timu nzima ya mabaunsa.
Akizungumza na wanahabari wakati alipowasili msanii huyo, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Matina Nkurlu alisema kuwa anafurahi kwa staa huyo kufika salama ndani ya nchi ya Tanzania sasa ni wapenzi tu wa burudani kukata tiketi kwa wingi ili waweze kushuhudia shoo hiyo. “Ninafurahi Ne-Yo amefika salama na mashabiki wa burudani wakate tiketi kwa wingi kadri iwezekanavyo ili waweze kuja katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza kesho na huduma mbalimbali kutoka Vodacom zitapatikana ndani ya uwanja huo,” alisema.
Shoo hiyo pia imedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.
A photo posted by NE-YO (@neyo) on

No comments: