Monday, 16 May 2016

MARK ZUCKERBERG AKUTANA NA SELENA GOMES KAMA STAR MWENYE FOLLOWERS WENGI INSTAGRAM..


Kwa mara ya kwanza mmiliki wa mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram Mark Zuckerberg amekutana na former X-Girl wa mwanamuziki Justin Bieber,Selena Gomes staa anaetajwa kuwa na followers wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram akiwa amejikusanyia jumla ya followers milioni 78.9 ila cha ajabu mrembo huyo account yake inaonesha kuwa she’s following only 247 peoples.

Zuckerberg mwenye umri wa miaka 31,ambae aliununua mtandao wa instagram mwaka 2012 kwa kiasi cha dola bilioni 1,huku mpaka sasa akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia kiasi cha dola bilioni 51.8,kupitia account zake za social media,Facebook & Instagram alipost picha akiwa na Selena Gomes na kuandika“Meeting with Instagram’s biggest star in our smallest room,Thanks for stopping,by Selena Gomez!”.
Achilia mbali post ya Bilionea huyo ambae mitandao yake imegeuka ugonjwa sugu kwa mamilioni ya watu duniani,Selena Gomes nae alipost picha akiwa Zuckerberg yenye ujumbe uliosomeka , “When you meet the boss and talk tech in a very unusual office.”aliandika Selena.
Mpaka sasa haijafahamika mkutano wa wawili hao ulihusu nini,ingawa baadhi ya wachambuzi wa masuala ya biashara duniani wanadai kuwa kutokana na Selena kuwa na idadi kubwa ya followers,pengine Zuckeberg anaweza kumtumia kama fursa ya kibiashara kwa ajili ya matangazo ya mitandao yake.

No comments: