Muigizaji Taraj P.Henson au maarufu kama Cookie kutokana na uhusika wake kwenye tamthilia ya Empire ni shabiki mkubwa wa wimbo wa ‘Caro’ wa Wizkid, ameandika kwenye Instagram yake.
“Who loves #WorldMusic #musichealsthesavagebeast ever since @tymwallacehair turned me and @ashuntasheriff on to this one!!!!!!! I hit play and dance like nobody’s watching”
Staa huyo wa Empire aliandika kwenye screenshot inayoonesha akisikiliza wimbo wa ‘Caro’ wa Wizkid kabla ya kumfollow kabisa Instagram.
Wizkid ametoboa kwenye soko la kimataifa tangu amshirikishe Drake kwenye Remix ya wimbo wake wa ‘Ojuelegba’ ambao amefanikiwa kuwashika mastaa wa Marekani kisawa sawa na sasa ameshirikishwa na Drake kwenye ‘One Dance’ wimbo ambao ni nambari moja kwenye chart za Billboard.



No comments:
Post a Comment