Amezungumza haya kuhusu Diamond Miaka miwili iliyopita, Rais Mstaafu Jakaya M. Kikwete alimkutanisha Diamond Platnumz na Rais wa zamani wa Def Jam, Kevin Liles.
Kevin Liles alikuwa Rais wa Def Jam Recordings na makamu mkuu wa Rais wa The Island Def Jam Music Group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004, Pia ni meneja wa Trey Songz, Big Sean na Estelle.
Baada ya kukutana, Diamond alisema kuwa aliunganishwa na Kevin Liles ili kumuongezea Connection zitakazo msaidia kuingiza muziki wake nchini Marekani, lakini hatukuwahi kusikia kutoka kwa Kevin Liles. Siku jana Meneja huyo wa Trey Songz na Big Sean alikuwa anajibu maswali ya mashabiki wake kupitia Twitter na aliulizwa kama anamsimamia Diamond au Diamond ana kazi ya msanii yoyote kati ya anaowasimamia,
Kevin Liles alijibu kuwa hamsimamii Diamond lakini ni rafiki yake mkubwa na tayari wanasaidiana kwenye mambo mbalimbali ambayo hakuyaweka wazi, hatahivyo hakujibu moja kwa moja kama Diamond amefanya kazi na wasanii waliopo chini yake.Is Tanzanian artist, Diamond Platnumz under your management or possibly working with any artist under your management? #AskKevinLiles— Sammie (@sammie_gratian) May 20, 2016
.@sammie_gratian #AskKevinLiles pic.twitter.com/CTgqZlttlq
— KevinLiles.com (@KevinLiles1) May 20, 2016


No comments:
Post a Comment