Tuesday, 28 June 2016

50 Cent apigwa faini ya $20k kwa lugha chafu.


Mahakama imempiga faini ya dola 20,000 rapper wa Marekani, 50 Cent kutokana na kitendo cha kutukana alichokifanya wakati wa tamasha la muziki lililofanyika St Kitts na Nevis, Caribbean.
50 Cent alifanya tukio hilo baada ya kuimba moja kati ya nyimbo zake zenye lugha ya matusi ndani yake na kuvunja sheria za visiwa hivyo vya Caribbean ambazo haziruhusu kutumia lugha za matusi hadharani.
Hata hivyo 50 Cent alikubali kosa hilo, na kulipa faini hiyo na kuweza kuachiwa huru.
Hivi karibuni 50 Cent amekuwa akikumbwa na kesi kadhaa ikiwemo ya hivi karibuni kushtakiwa yeye na Dr Dre na mtayarishaji wa muziki, Parrott kwa kitendo cha kutumia beat ya wimbo wa ‘P.I.M.P’ waliyocopy kutoka kwenye wimbo wake ‘BAMBA’ bila ya idhini.

No comments: