Tuesday, 28 June 2016

Chakujifunza kutoka kwenye tuzo za BET 2016


Hatimaye Juni 26 usiku zilifanyika tuzo za BET 2016 zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu kubwa hasa kwa watanzania kuweza kuona kijana wao, Diamond kama angeweza kuinyakuwa tuzo hiyo kwenye kipengele cha Best International Act: Africa iliyokwennda kwa Black Coffee wa Afrika Kusini.
Ni mwaka wa pili sasa Diamond amefanikiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo hizo, akianza mwaka 2014 na mwaka huu lakini kwa bahati mbaya mara zote hajafanikiwa kuipata tuzo hiyo. Tukumbuke kuna msemo unasema ‘Subira yavuta kheri’ labda zamu yetu bado haijafika.
Kwenye kipengele cha Best International Act: Africa watu tulikuwa tunatoa nafasi kwa wasanii wawili ambao tulitegemea kuwa ndiyo wangeweza kuchukuwa tuzo hiyo, Wizkid (Nigeria) na Diamond (Tanzania) lakini nafasi kubwa tulimpa Diamond kutokana na Wizkid hakuwahi kupost chochote kuhusu tuzo hizo wala kuomba kura kwa mashabiki wake lakini tulisahau kuwa kuna wasanii wengine sita nyuma yao wanawania tuzo hiyo.
Black Coffee hakupewa hata robo ya theluthi ya fikra na mawazo kama ataweza kuchukua tuzo hiyo kwa kuwa hafahamiki na mashabiki wengi na wengine hatukuwahi kumuona hapo kabla kwa kuwa tulishajengwa na fikra za Wizkid na Diamond ndiyo tunaofahamika kutokana na fan base yao kubwa waliojijengea kwenye muziki.
Kuteleza si kuanguka wala haitakiwi kukata tamaa kwa hili lililotokea pale Los Angeles usiku wa Juni 26, lakini linatakiwa liwe funzo na mwanzo mzuri wa kujifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya kwa kujiamini kupita kiasi na kuwachukulia poa wasanii wengine waliobaki kwenye kipengele kile kutokana na kutowafahamu vizuri kuwa CV zinaweza zikawa ni kubwa na nzuri zaidi ya Diamond na Wizkid.
Hatutakiwi kukata tamaa zaidi ya kuendelea kumpa support Diamond kutokana yeye ndiyo msanii pekee wa Tanzania aliyefanikiwa kufika kwenye tuzo hizo na ameweza kuuletea heshima kubwa muziki wa Bongo Fleva kwa kufahamika kwenye nchi nyingi, lakini pia ameweza kuchukua tuzo nyingi na kubwa duniani ikiwemo ya MTV EMA 2015 kwenye kipengele cha ‘Worldwide Act Africa/India’ aliyokuwa akishindana na Miss World mwaka 2000, Priyanka Chopra.

Msikilize/Angalia Diamond akiongelea hilo,

No comments: