Wednesday, 8 June 2016

mkwanja mrefu aliotoa Wiz Khalifa ilikukamilisha talaka kwa Amber Rose.


Wiz Khalifa na Amber Rose wamefikia makubaliano ya talaka yao na kwasasa wameachana mazima na kubaki marafiki tu. Kwa mujibu wa TMZ Amber amepokea dola laki sita na eflu arubaini na nne $644,000 ili kukamilisha dola milioni moja $1 million alizotakiwa kupewa.
Wiz Khalifa pia atakuwa anatoa dola $14,800 kila mwezi kwaajili ya malezi ya mtoto waomwenye miaka mitatu Sebastian ila watakuwa na haki sawa za malezi.
Wiz Khalifa atabaki na nyumba yake ya Pennsylvania na magari yote 10 waliyowahi kumiliki kama ’62 na ’64 Impalas, ’69 Chevelle, na ile ’68 Camaro.
Baada ya kumaliza makubaliano yao ya talaka Wiz na Amber Rose walienda kwenye club ya Ace of Diamonds mjini Los Angeles kula bata pamoja.

No comments: