Thursday, 15 March 2018

Waziri Mkuu aahidi kujizulu

Waziri Mkuu wa Slovakia  Robert Fico

Waziri Mkuu wa Slovakia  Robert Fico amesema kwamba yupo tayari kujiuzulu ikiwa rais wa nchi hiyo ataridhia kwamba serikali ya sasa ya muungano inaweza kuendelea mpaka mwisho wa muhula bila kuitisha uchaguzi wa mapema.

Waziri Mkuu Fico amesema yuko tayari kuwasilisha jina la Waziri Mkuu mpya kutoka chama chake.
Mtafaruku huo umeibuka baada ya kuibuka kwa kashfa ya kisiasa iliyosababisha kuwawa kwa mwandishi wa habariza uchunguzi nchini humo.
Mwandishi huyo wa habari Jan Kuciak alikuwa akifanya habari ya uchunguzi wa rushwa katika serikali hiyo lakini baadaye alikuja kuawa akiwa na mchumba wake Martina Kusnirova, waliposhambuliwa nyumbani kwao.
Waziri wa mambo ya ndani Robert Kalinak alijiuzuru siku mbili zilizopita kufuatia shinikizo kutoka kwa chama mshirika katika serikali hiyo cha The Most-Hid party.

No comments: